Omar al Bashir: Maandamano dhidi ya Rais wa Sudan yaendelea
Mamia ya watu wameandamana mashariki mwa mji wa Sudan wa al- Gadarif, huku maandamano ya dhidi ya Rais wa nchi hiyo Omar al Bashir yakiingia katika wiki ya tatu.
Mashuhuda wanasema kuwa majeshi ya ulinzi yametumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya kundi la watu, ambao walikuwa wakiimbia wakisema Uhuru, Amani na Mapinduzi kwa Sauti ya Wananchi.
- Omar el Bashir afanyiwa uchunguzi wa moyo
- ICC: Afrika Kusini ilistahili kumkamata Bashir
- Bashir: Ni rahisi kufanya kazi na Donald Trump
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Maprpfesa nchini Sudan, ambayo inamtaka Rais Bashir kujiuzulu.
Akizungumza katika kituo cha jeshi katika mji wa Atbara, kiongozi huyo amelaani kile alichokiita usaliti wa kuchoma mali kwa makusudi na kusababisha madhara.
Wakati huo huo Uingereza, Marekani, Canada na Norway zimetoa taarifa ya pamoja, zikisema kwamba zimeshtushwa na taarifa za vifo na kujeruhiwa kwa watu walioshiriki maandamano hayo ya kudai haki zao.
Taarifa hiyo imedai pia kusikitishwa na utumiaji wa silaha za moto unaodaiwa kufanywa dhidi ya waandamanaji.
Katika hatua nyingine maandamano ya kuiunga mkono serikali yanaweza kufanyika leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.
Maandamano ya kuipinga serikali kwa mara ya kwanza yalianza katikati mwa mwezi Desemba mwaka jana kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha.
Bei ya mkate ilipanda mara tatu katika baadhi ya maeneo na bei ya mafuta pia ikapanda.
No comments: