Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 09.01.2019: Gonzalo Higuain, Christian Eriksen, Koulibaly, Icardi, Luka Modric, Joe Hart, Ander Herrera
Chelsea wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Argentina Gonzalo Higuain, 31. (Marca)
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy anasema kiungo wa kati wa Denmark anayeichezea klabu hiyo Christian Eriksen, 26, thamani yake ni £225m . Mchezaji huyo amekuwa akitafutwa na Real Madrid. (AS)
Mshambuliaji Mhispania aliyechezea Tottenham zamani Fernando Llorente, 33, amepewa nafasi ya kurejea Athletic Bilbao. (Mirror)
Mkuu wa Athletic Bilbao Rafael Alkorta amethibitisha kwamba anamtaka kiungo wa kati wa Manchester United na Uhispania Ander Herrera, 29, arejee katika klabu hiyo. Herrera aliihama klabu hiyo ya Uhispaniamwaka 2014. (Cadena Ser, kupitia Mail)
Lakini huenda Herrera bado akasalia Old Trafford baada ya kaimu meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer kudaiwa kumshawishi asalie katika klabu hiyo. (Sun)
Manchester United wamekubali kwamba itawalazimu kusubiri hadi mwisho wa simu ndipo waweze kumpata beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (ESPN)
Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger ameombwa kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Qatar. (France Football)
- Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 04.01.2019
- Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 03.01.2019
- Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.01.2019
Inter Milan wako tayari kumuuza mshambuliaji wa Croatia Ivan Perisic, 29, kwa Manchester United ndipo waweze kupata pesa za kumnunua kiungo wa kati wa Real Madrid ambaye pia anatokea Croatia Luka Modric, 33. (Tuttosport, kupitia Calciomercato)
Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Mauro Icardi, 25, ni miongoni mwa wachezajia ambao mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anataka kuwanunua mwezi huu. (Mirror)
Bayern Munich wameongeza kitita ambacho wako tayari kutoa kumchukua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi hadi £35m. Mchezaji huyo wa miaka 18 amekariri hamu yake ya kutaka kuihama klabu hiyo ya Stamford Bridge mwezi huu. (Guardian)
Chelsea wanamtaka mshambuliaji wa AC Milan kutoka Ureno Andre Silva - ambaye yupo Sevilla kwa mkopo - lakini uhamisho huo utategemea the Blues kukubali mshambuliaji wao wa Uhispania Alvaro Morata ahamie klabu hiyo ya Sevilla. (Sun)
Everton wanamnyatia kiungo wa kati wa Porto na Algeria Yacine Brahimi na walimtuma skauti kumfuatilia Jumatatu wakati wa mechia ambayo walishinda 3-1 dhidi ya Nacional. Kiungo huyo wa miaka 28 alifunga mabao mawili mechi hiyo. (Mirror)
Kipa wa Burnley Joe Hart, 31, anatafutwa na klabu ya Preston ambao wanamtaka kwa mkopo. (Sun)
Crystal Palace wanamtaka mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham ajiunge nao kwa mkopo baada ya mchezaji huyo wa miaka 21 ambaye kwa sasa yupo Aston Villa kwa mkopo kukataa fursa ya kujiunga na Wolves. (Mirror)
Southampton wanataka sana kumsaini mshambuliaji wa Everton Ademola Lookman, 21. (Star - via HITC)
Fulham waliwatembeza beki wa England Gary Cahill, 33, winga wa Nigeria Victor Moses na kiungo wa kati wa England Danny Drinkwater, wote wawili wakiwa na miaka 28, katika uwanja wao wa mazoezi katika juhudi za kutaka kuwashawishi kujiunga nao kutoka Chelsea. (Love Sport Radio)
Beki wa Liverpool Rafael Camacho, 18, anatarajiwa kuondoka Anfield - siku chache tu baada yake kuchezeshwa mara ya kwanza katika timu kuu. Sporting Lisbon wanadaiwa kuwa karibu kuafikiana na Liverpool kuhusu beki huyo wa kulia. (Talksport)
Newcastle wanatafakari uwezekano wao wa kujiondoa kutoka kwenye mchakato wa kumnunua kiungo wa Atlanta United Miguel Almiron. Klabu hiyo ya St James' Park. inasema ujira anaodai mchezaji huyo wa miaka 24 kutoka Paraguay ni wa juu mno. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure amekiri kwamba anataka sana kuhamia kwa miamba wa Ufafaransa Paris St-Germain, ambao wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo wa miaka 26. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ubelgiji Mousa Dembele, 31, anakaribia kuhamia klabu ya Ligi Kuu ya China ya Beijing Guoan, uhamisho ambao utakuwa wa £11m. (Talksport)
Kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 25, anataka kuhamia Arsenal mwezi hu wa Januari, ingawa klabu yake awali haikutaka kumwachilia. (Mirror)
Spurs wanatarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wao kutoka Uholanzi Vincent Janssen ambaye amekuwa hachezeshwi sana, na wanataka kumwacha mshambuliaji huyo wa miaka 24 aondoke Januari. (Mail)
Beki wa kati anayechezea Burnley Jimmy Dunne, 21, anatafutwa na Sunderland kwa mkopo. (Burnley Express)
Reading wamekataa ofa ya £450,000 kutoka Wigan ambao wamekuwa wakimtaka beki Tyler Blackett, 24. (Mail)
Preston na West Brom wote wanamtaka kiungo wa kati wa Mansfield CJ Hamilton, 23. (Mansfield Chad)
Newcastle wamekataa ofa kutoka kwa West Brom ambao wamekuwa wakimtaka kiungo wa kati Isaac Hayden, 23. (Express & Star)
Aston Villa pia wanadaiwa kujitosa katika mbio za kumtaka Hayden. (Mirror)
Arsenal wanatafakari uwezekano wao wa kumteua kiungo wa kati wa zamani Edu kuwa mkurugeniz wao mpya wa uchezaji. Mbrazil huyo alistaafu soka mwaka 2010. (Standard)
Barcelona wako radhi kumuuza winga wao kutoka Brazil Malcom, 21, ingawa walimnunua majira ya joto yaliyopita. (Mundo Deportivo)
Tottenham wanamfuatilia kwa karibu beki kamili wa Wolves Matt Doherty ingawa mchezaji huyo wa miaka 26 huenda akaongezewa ujira wake maradufu katika klabu hiyo ya Molineux wiki chache zijazo. (Irish Independent)
West Ham wanatarajiwa kuimarisha ofa yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa zamani wa Cardiff Gary Medel. Mchezaji huyo wa miaka 31 kutoka Chile anatarajiwa kuihama Besiktas iwapo kutatokea klabu iliyo tayari kutoa pesa zinazofikia makadirio ya thamani yake. (Takvim - kupitia Sport Witness)
Bora kutoka Jumanne
Manchester United wameanzisha mazungumzo na Barcelona wakitaka kumsajili mshambuliaji Mbrazil Philippe Coutinho, 26, lakini ndipo waweze kumnasa itabidi wachomoe zaidi ya £100m. (Caught Offside)
Sevilla wamefanya mazungumzo na Chelsea kuhusu kumchukua mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 26, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Goal.com)
AC Milan wanamtafuta mshambuliaji wa Genoa na Poland Krzysztof Piatek, 23, wakitaka kumtumia kujaza pengo litakaloachwa na mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuan, 31. (La Gazzetta dello Sport)
Uhamisho wa Cesc Fabregas kwenda Monaco unakwamishwa na hali kwamba klabu hiyo ya Ligue 1 bado haijaafikiana na klabu ya Chelsea kuhusu ada ya uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Uhispania mwenye miaka 31. (London Evening Standard)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemshauri Fabregas kuihama klabu hiyo ya Stamford Bridge kwa maslahi ya uchezaji wake. (Talksport)
Juventus wanasema wanaweza wakashawishika kumuuza Paulo Dybala, 25, ambaye anatafutwa na Manchester City mwisho wa msimu, lakini mradi tu ada ya uhamisho wa raia huyo wa Argentina iwe zaidi ya £90m. (Tuttosport kupitia Express)
Atletico Madrid wamekataa ofa kutoka kwa Manchester United waliokuwa wanamtaka beki wa Uruguay Diego Godin, 32. (Tutto Mercato Web)
Beki wa Ajax anayechezea timu ya taifa ya Uholanzi Matthijs de Ligt, 19, amehimizwa kukataa kuhamia Juventus na badala yake ajiunge na Manchester United. (Manchester Evening News)
Real Madrid wameanza harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Denmark Christian Eriksen, 26, kutoka Tottenham na wanajiandaa kutoa takriban £100m kumnasa. (Independent)
No comments: