Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 31.12.2018: Isco, Pepe, Holgate, Hudson-Odoi, Solanke, Bakayoko
Kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 26, amepuuzilia mbali uwezekano wake wa kuhamia klabu ya Chelsea ya England. Amesema hataondoka Bernabeu wakati wa kipindi cha kuhama wachezaji Januari. (Deportes Cuatro, kupitia Metro)
Manchester City wanamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Real Betis Junior Firpo lakini wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid ambao pia wanataka saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Mirror)
Mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke, 21, amefanyiwa vipimo vya matibabu katika klabu ya Crystal Palace huku akikaribia kuhamia Selhurst Park kwa mkopo. (Mail)
Winga wa klabu ya Lille ya Ufraansa Nicolas Pepe mwenye miaka 23 ambaye amehusishwa na Arsenal, Barcelona na Manchester City, anaonekana kuwa tayari kuhama mwisho wa msimu. (Le Voix du Nord, kupitia Star)
Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko, 24, amesema yuko radhi kusalia AC Milan hata baada ya kipindi chake cha kuwa na klabu hiyo ya Italia kwa mkopo wa msimu mmoja kukamilima mwisho wa msimu. (MilanNews, kupitia Mail)
West Brom wanakaribia kutia saini mkataba na beki wa Everton Mason Holgate, 22, kwa mkopo Januari. (Express na Star)
Klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani imejitosa kwenye mbio za kutaka kumnunua winga wa Chelsea mwenye miaka 18 Callum Hudson-Odoi. (Kicker - German)
Mchezaji anayenyatiwa sana na Liverpool ambaye kwa sasa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 20, anaonekana kukaribia kujiunga na Chelsea kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na msambuliaji wa zamani wa Marekani Eddie Johnson kwenye mitandao ya kijamii. (Calciomercato)
Middlesbrough wanatumai wataweza kumsaini kiungo wa kati wa Huddersfield Rajiv van La Parra, 27, kwa mkopo kukiwa na uwezekano wa kumchukua kwa mkataba wa kudumu baadaye mwisho wa msimu. (Yorkshire Post)
Meneja Brendan Rodgers amesema Celtic wana kazi kubwa ya kufanya sokoni Januari kuwanunua wachezaji wapya. (Irish Times kupitia Celtic TV)
Meneja msaidizi wa timu ya taifa ya England Steve Holland amesema timu hiyo haikujiandaa na kucheza nusufainali yao ya Kombe la Dunia Urusi ilivyofaa. (Telegraph)
Bora kutoka Jumapili
Chelsea wametoa ofa ya hadi pauni milioni 45 kumsaini mshambuliaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic msimu ujao lakini klabu hiyo ya Ujerumani itacheleweza uamuzi wake inaposubiri ofa kutoka kwa vilabu vingine kwa mchezaji huyo raia wa Marekani mwenye miaka 20. (ESPN)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumwendea straika wa Leeds Kemar Roofe, 25, ikiwa atapewa pesa mwezi Januari. (Sunday Mirror)
Meneja wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amewashauri kipa wa Uhispania David de Gea, 28, na mshabuliaji Mfaransa Anthony Martial, 23, kusaini mikataba mipya na klabu hiyo. (Mail on Sunday)
Chelsea wameambiwa kuwa ni lazma walipe pauni milioni 30 ikiwa wanataka beki mjerumani Mats Hummels, 30, mwezi Januari. (Sun on Sunday)
Cardiff wanaongoza mbio za kumwinda beki wa Liverpool Nathaniel Clyne, licha ya Fulham na Leicester nao kuwa na nia ya kumsaini kiungo huyo wa miaka 27 raia wa England. (Sunday Mirror)
Mlinzi wa Manchester United raia wa Italia Matteo Darmian, 29, analengwa na Inter Milan na Lazio. (Calciomercato)
No comments: