sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Comments

Text Widget

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Total Pageviews

Translate

Advertise

Comments


Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Column Left

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Recent Posts

Popular Post

Most Popular

Recent Tube

Wisata

News Scroll

Favourite

Event

Culture

Gallery

GEORGE WAEH WARUDI IKULU

Rais wa liberia arejea ofisini wiki mbili baada ya kufurushwa na nyoka




Jengo hilo lilitakiwa kusafishwa vizuri kwa kemikali ya kuua nyoka kabla rais kushauriwa kurejea ofisini kwake JumatanoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Rais wa Liberia na nyota wa zamani wa soka George Weah, amerejea tena kazini , wiki mbili kamili baada ya kuitoroka ofisi yake kwasababu nyoka wawili walikuwa wamepatikana katika jengo la ofisi yake.
Jengo hilo lilitakiwa kusafishwa vizuri kwa kemikali ya kuua nyoka kabla rais kushauriwa kurejea ofisini kwake Jumatano.
Mmoja wa watu wa kwanza kumtembelea rais Weah katika ofisi yake alikuwa ni Makamu rais wa zamani Joseph Boakai, aliyeshindwa na Weah katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.
Bwana Weah alizungumzia juu ya juhudi za serikali yake za ''kulinda misingi ya demokrasia'', na kuwavutia wawekezaji wa kigeni iki kuinua uchumi, taarifa hiyo ilitumwa kwenye wavuti wa serikali.
Rais amekuwa akifanyia kazi katika ofisi iliyopo ghorofa ya sita ya jengo la Wizara ya mambo ya nje tangu jengo jirani na ofisi ya rais lilipoungua kwa moto mwaka 2006.
Nyoka wawili weusi ambao walitoka kwenye shimo lilolokuwa kwenye sehemu ya mapokezi ya jengo la ghorofa sita walikwenda nyuma ya jengo hilo ghafla wakati watu walipokuwa wakijaribu kuwauwa.
Baada ya tukio hilo maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa rais walionekana wakiyalinda makao ya Bwana Weah katika mji mkuu wa Monrovia.
Kanda ya video iliochapishwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la African News ilionyesha wafanyikazi wakijaribu kushambulia nyoka wakati walipoonekana katika eneo la kukaribisha wageni la jengo hilo.
Jumba hilo limekuwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa sasa kwasababu yamfumo wa maji taka , na maafisa wanasema kuna uwezekano wa nyoka kuingia katika jumba hilo.
Haijafahamiika ikiwa nyoka hao waliuawa au la.

MLINZI WA MFALME KUWA MKE WAKE

Mfalme wa Thailand Vajiralongkorn amemuoa mlinzi wake na kumtawaza kuwa Malkia




Picha iliyotolewa na ofisi ya Ufalme wa Thailand inaonyesha Mfalme wa Thai Maha Vajiralongkorn Bodindradebayavarangkun ( Kulia )akimmwagia maji Generali Suthida Vajiralongkorn na AyudhyaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMfalme anaonekana akimwaga maji ya baraka kwenye kichwa cha Malkia Suthida

Mfalme wa Thailand amemuoa Naibu mkuu wa kikosi cha walinzi wake , na kumpa cheo cha malkia, imesema taarifa ya ufalme huo.
Tangazo hilo la kushitukiza limetolewa huku sherehe za kutawazwa kwake zikitarajiwa kuanza Jumamosi, wakati atakapochukua wadhfa wake.
Mfalme Maha Vajiralongkorn, mwenye umri wa miaka 66, alikuwa mfalme kikatiba baada ya kifo cha baba yake aliyependwa sana kilichotokea mwaka 2016.
Amekwisha wataliki wanawake mara tatu na ana watoto saba
Ufalme ulisema kuwa: Mfalme Vajiralongkorn "ameamua kumpandisha cheo Generali Suthida Vajiralongkorn Na Ayudhya, na kuwa Malkia Suthida na atakuwa na cheo cha kifalme na hadhi kama sehemu ya sfamilia ya kifalme".
Malkia Suthida ni mpenzi wa muda mrefu wa Mfalme Vajiralongkorn na amekuwa akionekana hadharani pamoja nae kw amiaka mingi, ingawa mahusiano yao haukuwahi kukubalika rasmi.


King Maha Vajiralongkorn na mpenzi wake , Generali Suthida Vajiralongkorn ambaye ametajwa kuwa Malkia Suthida katika harusi yao mjini Bangkok, Thailand Mei 1, 2019, kHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMalkia Suthida alipewa cheo cha Generali mwaka 2016

Picha kutoka kutoka katika sherehe za harusi zilionyeshwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni vya Thailand Jumatano, ambapo watu wa wengine wa familia ya ufalme na washauri wa ufalme walihudhuria.
Mfalme alionekana akimwagia maji ya baraka Malkia Queen Suthida kichwani. Baadae wawiloi hao walisaini cheti cha ndoa.
Mnamo mwaka 2014 Vajiralongkorn alimteua Suthida Tidjai, ambaye ni mhudumu wa zamani wa Thai Airways,kama naibu kamanda wa kikosi cha walinzi wake. Alimpandisha cheo na kuwa Generali kamili jeshini Disemba 2016.
Mfalme aliyetangulia Bhumibol Adulyadej, alitawala kwa miaka 70 na kuwa ndiye mfalme aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani na alifariki dunia mwaka 2016

Uchaguzi Ukraine : Mchekeshaji Zelensky ashinda nafasi ya urais

Uchaguzi Ukraine : Mchekeshaji Zelensky ashinda nafasi ya urais



Volodymyr ZelenskyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUcheshi wa Volodymyr Zelensky katika filamu fupi umeweza kumsaidia kuwa rais

Mchekeshaji wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa urais , kutokana na kura zilizopigwa.
Kura hizo zimempa nafasi mwanasiasa mpya ambaye amechaguliwa kwa kuungwa mkono na zaidi ya asilimia 70.
Bwana Zelensky mwenye umri wa miaka 41, ameweza kumtoa madarakani rais Petro Poroshenko ambaye amekubali kushindwa.
Matokeo ya sasa yanaonekana kuwa ni pigo kubwa kwa bwana Poroshenko na kukataliwa kuanzishwa kwa Ukraine mpya.
"Sitawaangusha ," Bwana Zelensky aliwaambia waliomuunga mkono wakati wa sherehe za kujipongeza.
Aliongeza kusema "Sijawa rais bado lakini kama raia wa Ukraine, ninaweza kuwaambia nchi zote za Kisovieti kuwa watuangalie sisi, Kila kitu kinawezekana !"
"Kama kura ziko sawa, basi atakuwa amechaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano". Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa hapo baadae.
Zelensky anajulikana kwa umahiri wa ucheshi wake kama muigizaji nyota wa mfululizo wa filamu ya satirical katika television ambapo anaigiza kama rais wa Ukraine.
Rais ana mamlaka makubwa katika upande wa usalama, jeshi na sera za kigeni katika nchi hiyo.

Presentational grey line

Aibu ya Poroshenko

Petro PoroshenkoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPetro Poroshenko

Uchaguzi wa Ukraine unaangalia mwanasiasa mwenye ujuzi wa miaka mitano katika urais na katika wasifu wa mchekeshaji aliyeshinda hana ujuzi zaidi ya karatasi tu.
Watu wengi wamempigia kura Volodymyr Zelensky ambapo ni aibu kubwa kwa Petro Poroshenko.
Wagombea thelathini na saba waliondolewa kwenye karatasi ya uchaguzi kutoka pande zote za kwanza na bado rais alichukua kura zaidi ya asilimia 9 wakati huu na bwana Zelensky alipata karibu asilimia 45.
Hii inaonyesha kuwa kura nyingi zilipigwa kwa ajili na timu yake ya kampeni iliyokuwa inasheherekea.
Aidha ni ngumu kuona hisia hizo kudumu kwa muda. Kazi kubwa inakuja pale utekelezaji unapoanza .
Ni jambo moja kuwa na wazo lakini jambo lingine ni utekelezaji.

Presentational grey line

Kura zilimpa ushindi wa urais bwana Poroshenko, mwaka 2014 kwa asilimia 25 za kura.
"Matokeo ya urais yanatuacha njia panda", alisema baada ya kura kutangazwa.
Bwana Poroshenko aliongeza, "Nitatoka madarakani lakini sitaacha siasa."

Presentational white space

Volodymyr Zelensky ni nani?
Zelensky amekuwa akicheza mchezo wa kuigiza inayoitwa 'Servant of the People ' ambapo kwa bahati tu akawa muigizaji anayetaka kuwa rais wa Ukrainne.
Anacheza kama mwalimu ambaye aliyechaguliwa baaada ya kufukuzwa kwa kosa la rushwa kusambaa katika mitando ya kijamii.
Aligombea nafasi ya urais kwa jina la chama cha siasa ambacho ni sawa na kipindi chake cha televisheni.

Volodymyr ZelenskyHaki miliki ya pichaEPA
Image captionVolodymyr Zelensky amehaidi kupambana na rushwa

Akiwa hana uzoefu wowote wa siasa ,wkampeni za Zelensky ziliangazia utofauti wake na wagombea wengine badala ya mawazo ya sera.
Awamu ya kwanza alishinda kwa asilimia zaidi ya 30 za kura ambapo zilikuwa ni mara mbili ya mpinzani wake Poroshenko ambaye alikuwa na asilimia 15.

MARTIN FAYULU AVUNJA UKIMYA JUU YA MATOKEO YA UCHAGUZI DRC

Mgombea wa upinzani Martin Fayulu ameonya tume ya uchaguzi kutoficha ukweli



Martin Fayulu, mgombea wa upinzani akizungumza na wanahabari mjini Kinshasa, Democratic Republic of Congo, 8 January 2019Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMartin Fayulu, mgombea wa upinzani anasema mamlaka sharti itangaze matokeo ya uchaguzi ili kuzima taharuki inayoshuhudiwa nchini

Mgombea wa urais wa upinzani nchini Congo DRC Martin Fayulu amewaonya maafisa wa uchaguzi dhidi ya ''kuficha ukweli'' huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda baada ya matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa.
Bwana Fayulu amesema "watu wa Congo tayari wanajua" matokeo ya uchaguzi uliyofanyika Desemba 30 kuahirishwa kwa wiki moja.
Matokeo ya awali ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa siku ya Jumapili ya Januari 6 lakini yakaahirishwa.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kumtafuta mrithi wa rais Joseph Kabila, ambaye anaachia madaraka baada ya kuongoza nchi hiyo ya maziwa makuu kwa miaka 18.
Kabila ameahidi kwamba uchaguzi huo ambao ulikuwa umepangwa ufanyike miaka miwili uliyopita utakuwa wa kwanza wa kupokezana madaraka kwa njia ya kidemokrasia nchini DR Congo tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1960.
Mrithi wake anayempendelea ambaye pia ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Shadary,anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa upinzani Martin Fayulu,tajiri mkubwa wa mafuta na Felix Tshisekedi, mwana wa kiume wa kigogo wa upinzani.

Afisa wa tume ya uchaguziHaki miliki ya pichaREUTERS

Siku wa Jumanne, Bwana Fayulu alisema Tume ya uchaguzi (Ceni) lazima "itangaze matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais hivi karibuni," akiongeza kuwa: "Matokeo ya uchaguzi kamwe haina mjadala."
Awali mkuu wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa, alisema kuwa kura kutoka baadhi ya vituo vya kupigia kura bado hazijahesabiwa.
Bwana Nangaa, ambaye hajasema nilini matokeo ya awali yatatangazwa ametoa wito kwa watu kuwa na subira licha ya hali ya wasiwasi inayoendelea kushuhudiwa nchini kutokana na kucheleshwa kwa matokeo ya uchaguzi.
Huku hayo yakijiri kanisa katoliki ambalo lilitoa jumla ya waangalizi 40,000 limesema kuwa linajua ni nani aliyeshinda uchaguzi.
Tamko hilo limekosolewa vikali na maafisa wa serikali ya bwana Kabila.
Siku moja baada ya uchaguzi huduma ya mawasiliano ya intaneti yalifungwa katika miji muhimu ya taifa la DR Congo katika hatua ambayo serikali ilesema ni ya kudhibiti kusambazwa kwa matokeo ya uchaguzi amabyo sio rasmi
Mwezi uliyopita rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa wanajeshi 80 wa nchi hiyo wamepelekwa katika taifa jirani la Gabon ili kuwapa ulinzi raia wake nchini DRC endapo ghasia zitatokea baaada ya uchaguzi..

Presentational grey line

Waliyogombea urais ni kina nani?
Kulikuwa na jumla ya wagombea urais 21 lakini wagombea wakuu ni watatu:

Martin FayuluHaki miliki ya pichaREUTERS

  • Martin Fayulu, Mkurugenzi mkuu wa zamani wa mafuta ambaye ameahidi nchi yenye mafanikio lakini ambaye watu maskini wanahisi hawezi kuwatetea.

• Emmanuel ShadaryHaki miliki ya pichaAFP

  • Emmanuel Ramazani Shadary, Waziri wa zamani wa mambo ya ndani na mtiifu kwa Kabila, ambaye aliwekewa vikwazo na Muungano wa Ulaya kwa hatua zilizochuliwa upinzani wakati wa maandamano ya mwaka 2017.

Felix TshisekediHaki miliki ya pichaREUTERS

  • Felix Tshisekedi Tshilombo, Mtoto wa mwanasiasa mkongwe ambaye ameahidi kupambana na umaskini.

Presentational grey line

Zaidi kuhusu DR Congo

Nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati ina utajiri wa madini na ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya cobalt, yanayotumiwa kwa simu na betri za magari.
Rais Kabila alichukua nafasi ya uongozi baada ya baba yake Laurent Kabila kuuawa mwaka 2001.
Alichaguliwa rasmi mwaka 2006, na baadae akapata tena nafasi ya kuongoza kwa muhula mwingine baada ya uchaguzi mwa mwaka 2011 uliyokumbwa na utata.
Alizuiliwa kugombea tena urais baada ya muhula wake wa mwisho uongozini kukamilika.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo rais Kabila alitakiwa kuachia madaraka miaka miwili iliyopita , lakini uchaguzi uliahirishwa baada ya tume ya uchaguzi kusema kuwa inahitaji muda zaidi kuwasajili wapiga kura.

Uongozi wa Congo DRC tangu ilipojinyakulia uhuru mwaka 1960 kutoka kwa Ubelgiji

YALIYOJILI MUDA HUU KUHUSU UCHAGUZI WA DRC J'PILI

Uchaguzi DRC: Mamlaka huenda zikaahirisha uchaguzi wa Jumapili

Sambaza habari hii Messenger


Wafuasi wa Fayulu

Mamlaka za uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) zimasema huenda uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika siku ya Jumapili ukahairishwa.
Msemaji wa tume ya uchaguzi DRC CENI Jean-Pierre Kalamba ameiambia BBC kuwa uchaguzi huo huenda ukasogezwa mbele kwa siku kadhaa kutokana na kile kinachotajwa kama maandalizi ambayo hayajakamilika.
Mchana wa leo Desemba 20, tume hiyo inatarajiwa kukutana na wanahabari na jambo jilo linatarajiwa kutolewa ufafanuzi.
Uchaguzi wa DRC umekuwa ukisogezwa mbele kwa zaidi ya miaka miwili sasa, huku rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila akishutumiwa kwa kutoa visingizio kadhaa vya kuahirisha uchaguzi ili aendelee kusalia madarakani.
Wiki iliyopita ghala la tume ya uchaguzi liliopo jijini Kinshasa liliteketea kwa moto na kuunguza baadhi ya vifaa muhimu vya uchaguzi, hata hivyo, mamlaka ziliwahakikishia wananchi kuwa moto huo hautaathiri kufanyika kwa uchaguzi.

Mamlaka zilidai kuwa moto uliozuka kwenye ghala la tume ya uchaguzi hautazuia uchaguzi wa Disemba 23.Haki miliki ya pichaCENI
Image captionMamlaka zilidai kuwa moto uliozuka kwenye ghala la tume ya uchaguzi hautazuia uchaguzi wa Disemba 23.

"Tumewaambia mafundi wetu ya kwamba wafanye juhudi zao zote ili uchaguzi ufanyike Disemba 23, lakini kila wakati tunaangalia wapi walipofika. Kama haiwezekani tunapanga kuongea na wanasiasa ili kuangalia namna gani tutaweza kuahirisha uchaguzi na kuongeza siku nne, saba au 14 na sioni wapi kuna ubaya wakati tunataka kufanya mambo kwenye utaratibu mzuri," amesema Kalamba.
Tanganzo hilo la ghafla linatokea wakati polisi wamemzuia mmojwapo wa wagombea wakuu wa upinzani wa kiti cha urais Martin Fayulu kuzindua kampeni zake katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Alipokuwa kizuizini Fayulu ameiambia BBC kuwa hatakubali uchaguzi uahirishwe hata kwa sekunde.
"Hatuwezi kukubali kukubali kuahirishwa kwa uchaguzi kwa namna yeyote ... (rais Joseph) Kabila amefahamu kuwa mimi naitwa mwanajeshi wa raia, ikiwa tarehe 23 hakuna uchaguzi kabila na mkuu wa tume huru ya uchaguzi wanapaswa kuondoka," amesema Fayulu.
Kama kweli uchaguzi utaahirishwa, kuna kila dalili ya kutokea kwa machafuko ya kisiasa na makabiliano kati ya raia na vyombo vya usalama.
Uchaguzi huu ukifanikiwa kufanyika itakuwa ndiyo mara ya kwanza kwa DRC kushuhudia mabadiliko ya uongozi kwa njia ya amani.

Kuzuiwa Kampeni


Polisi walilazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa upinzani baada ya kuzuia mkutano wao wa kampeni
Image captionPolisi walilazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi wafuasi wa upinzani baada ya kuzuia mkutano wao wa kampeni

Mamlaka za jiji Kinshasa zilitangaza marufuku ya kufanyika kwa shughuli za kampeni kuanzia jana katika jiji hilo kuu la nchi ikiwa ni muda mchache tu kabla ya Fayulu kuzindua kampeni zake.
Licha ya tangazo hilo, maelfu ya wafuasi wa Fayulu walijitkeza kwenye uwanja ambao ulipangwa kufanyika kwa mkutano wao.
Hata hivyo, Fayulu alizuiwa na polisi takribani kilomita 50 mbali na uwanja huo na kumfanya kushindwa kufika na kuhutubia na kumwaga sera mbele ya wafuasi wake.

Vurugu
Image captionVurumai zilizuka baada ya mkutano wa mgombea wa upinzani Martin Fayulu kuzuiliwa

Gavana anayeegemea upande wa serikali wa mji wa Kinshasa Andre Kimpita, alisema kuwa hatua hiyo ya kupiga marufuku mikutano ya siasa imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.
Hatua hiyo haikupokelewa vyema na wafuasi wa Fayulu ambao waliingia barabarani na kuandamana wakitishia vurumai iwapo Fayulu hatakabidhiwa mamlaka baada ya uchaguzi.
Polisi iliwalazimu kutumia nguvu ya ziada kuwatawanya wafuasi hao wa Fayulu kwa kuwarushia mabomu ya machozi.