Romelu Lukaku: Mkufunzi wa Man Utd Jose Mourinho 'hawezi kuficha hisia zake'
Jose Mourinho hadanganyi na hawezi kuficha hisia zake kama wakufunzi wenzake katika ligi ya Uingereza , kulingana na mshambulijia wa United Romelu Lukaku.
Mkufunzi wa United Mourinho alitaka kupewa heshima na vyombo vya habari baada ya kukasirika katika mkutano na wanahabari baada ya timu yake kupoteza 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham mwezi Agosti.
Lakini Lukaku anasema kuwa raia huyo wa Ureno ni mtu wa familia , ''huwafanya wachezaji kucheka na anawapigania'' , hivyobasi anahitaji heshima.
''Watu wanajua kwamba ana upande unaomfanya kuwa mshindi'', alisema Lukaku.
''Lakini kile ninachompendea hawezi kuficha hisia zake. Wakati anapokasirika utajua amekasirika, anapofurahi utajua anafurahi''.
''Sijui kwa nini watu hawapendi ukweli kumuhusu. Wakati anaponikasirikia najua kwamba amenikasirikia hivyobasi najaribu kufanya anachotaka hatua inayomfanya kufurahi tena.
Katika mahojiano na Dion Dublin , mshambuliaji huyo wa Ubelgiji pia amezungumnzia kuhusu mafunzo aliopata kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Ufransa na Arsenal pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba , mbali na uhusiano wake na mkufunzi wa zamani wa Everton Ronald Koeman huku akitaka kumaliza kazi yake bila majuto yoyote.
'Mourinho anependwa na kila mtu'
United ilimaliza ya pili katika jedwali la ligi ya Uingereza msimu uliopita lakini ilipoteza mechi mbili za kwanza kati ya nne katika kampeni yao.
Lukaku ,25, anasema kuwa Mourinho hatosita kuingilia kati iwapo hafurahii wachezaji wanavyocheza ama timu yote kwa jumla.
''Mara nyengine wachezaji tunakuwa laini sana'' , aliongezea Lukaku.
''Ninapowasikiliza wachezaji wa zamani na wa sasa , mkufunzi hawezi kusema anachotaka kutoka kwa mchezaji kwa sababu unahisi anakushambulia''.
''Lakini sihisi ananishambulia, kwasababu hivyo ndivyo nilivyo-mimi sio laini, lakini huwezi kupata nguzo kama hiyo katika soka -ninakotoka ndivyo tulivyo''.
''Uhusiano wangu naye ni mzuri . Ananichekesha , anawafanya wachezaji kucheka ni mtu anayependa familia''.
Lazima watu waheshimu kwamba anataka kujihifadhia heshima yake. Hapa anataka tuimarike . Ni mtu wa kawaida, tuna uhusiano mzuri naye anapendwa na kila mtu.
No comments: