sponsor

sponsor

Slider

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Comments

Text Widget

Sample Text

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Ut enim ad minim veniam, quis nostrud exercitation test link ullamco laboris nisi ut aliquip ex ea commodo consequat.

Contact Form

Name

Email *

Message *

Total Pageviews

Translate

Advertise

Comments


Definition List

Definition list
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.
Lorem ipsum dolor sit amet
Consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

Support

Need our help to upload or customize this blogger template? Contact me with details about the theme customization you need.

Ordered List

  1. Lorem ipsum dolor sit amet, consectetuer adipiscing elit.
  2. Aliquam tincidunt mauris eu risus.
  3. Vestibulum auctor dapibus neque.

Column Left

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Vivamus leo ante, consectetur sit amet vulputate vel, dapibus sit amet lectus. Etiam varius dui eget lorem elementum eget mattis sapien interdum. In hac habitasse platea dictumst.

Recent Posts

Popular Post

Most Popular

Recent Tube

Wisata

News Scroll

Favourite

Event

Culture

Gallery

» »Unlabelled » VILIO NA MAJONZI VYA ENDELEA KUTANDA NCHINI KENYA: Fahamu sababu tano kwanini majengo yanaporomoka

 Sababu tano za kwanini majengo yanaporomoka zabainishwa




Haki miliki ya picha EPA
Image caption Watu wengi wanahofiwa wamekwama chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka

Saa kadhaa baada ya jumba la ghorofa sita kuanguka katika eneo la Tassia, viungani mwa jiji la Nairobi nchini Kenya.
Inaaminika watu 46 walikuwa wakiishi katika jengo hilo, lakini ghorofa ya chini haikuwa na watu.
Kufikia sasa haijafahamika ni watu wangapi walionaswa chini ya vifusi vya jengo hilo lililoporomoka.
Gumzo tayari limeibuka katika mitandao ya kijamii kuhusu usalama wa majengo ya makaazi jijini humo.

Lakini je, nyumba zinazojengwa ziko katika hali gani?

1. Msingi wa nyumba ni dhaifu

 Watu wanahofiwa kunasa kwenye kifusi

Kujenga msingi ulio imara ni gharama mno.
Inasemekana kwamba gharama yake inaweza kuwa nusu ya pesa utakazotumia katika ujenzi, hayo ni kulingana na profesa wa uhandisi wa majengo Anthony Ede wa chuo kikuu cha Covenant, Ota, Nigeria.
Alisema kwamba kuna mambo mawili ambayo ni lazima yazingatiwe wakati unajenga msingi wa nyumba - uimara wa udongo na uzito wa jengo.

Haki miliki ya picha Dickson Omari
Image caption Watu wanahofiwa kunaswa kwenye kifusi cha jumba lililoporomoka Tassia, katika eneo la Embakasi Nairobi
Katika mji wa Lagos, Nigeria eneo lenye majimaji linahitaji msingi imara tofauti kabisa na eneo ambalo ni imara.
Lakini bwana Ede anasema wamiliki hutaka sana kubana matumizi bila kuzingatia sehemu wanazo jenga na matokeo yake ni kwamba majengo mengi mjini Lagos yameporomoka.
Hata hivyo, maeneo ambayo ni imara pia yanahitaji msingi thabiti.
Kulingana na wachunguzi, msingi unaotetereka ni moja ya sababu tatu zilizochangia kuanguka kwa jengo la ghorofa nne kaskazini mwa Rwanda na kusababisha vifo vya watu mwaka 2013.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Zaidi ya watu 30 waliokolewa baada ya jengo moja kuporomoka huko Nyagatare, kaskazini-mashariki mwa Rwanda mwaka 2013 
Kifaa kikitoa vifusi katika jengo lililoporomoka huko Nyagatare, kaskazini mashariki mwa Rwanda Mei 15, 2013. Watu sita waliaga dunia huku wenguine kadhaa wakijeruhiwa. Polisi na jeshi walishirikiana walishirikiana kuondoa walionaswa na watu karibia 30 wakaokolewa wakiwa hai. AFP PHOTO /Stephanie Aglietti

2. Nyenzo zinazotumiwa katika ujenzi siyo imara.

Vifaa visivyoweza kuhimili uzito ndio vinavyotumika, amesema Hermogene Nsengimana kutoka shirika la African Organization for Standardisation, ambalo liliwahi kuhudhuria mkutano uliofanyika mjini Nairobi na kujadili majengo mengi yanayojengwa Afrika yanaporomoka.
Nsengimana alisema kwamba kuna soko la vifaa ghushi na wakati mwingine vyuma vikuukuu vinatumika badala ya vyuma vinavyohitajika.
Wakati jumba la ghorofa sita lililoporomoka mjini Kampala, Uganda mnamo mwezi Aprili, Mkurugenzi wa mamlaka ya mji alisema kwamba jengo hilo lilikuwa limejengwa kwa kutumia vifaa bandia.
Bwana Nsengimana alisema pia kuna visa vya vifaa ghushi kuuzwa kama nyenzo halisi.
Lakini akasema kwamba wanakandarasi pia nao wakati mwingine hutumia vifaa bandia wakiwa na ufahamu wa hilo ili kupunguza gharama.
Kwa hivyo wanaweza kutumia zege inayotatikana katika ujenzi wa ghorofa moja kwa jengo la ghorofa nne.
Bwana Ede aliongeza kuwa hili ni miongoni mwa yale ambayo wadhibiti wanatakiwa kuunda sera zake.
 Watu wakiokolewa katika jengo moja mjini Kampala

Image caption Timu ya uokozi iliyokuwa ikiwaokoa walionaswa katika jengo la ghorofa sita mjini Kampala mwezi Aprili
3. Wafanyakazi hufanya makosa
Wakati mwingine hata wafanyakazi wanapopewa nyenzo stahiki za kutengeneza zege, huchanganya vibaya, Edo anasema.
Na hilo husababisha uwepo wa zege ambayo si imara kwa jengo husika.
Bwana Edo alilaumu wahandisi wanaopunguza gharama kwa kuajiri wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi kwa sababu malipo yao ni ya chini ukilinganisha na wale waliosomea kazi hiyo.
Hii ndiyo moja ya sababu iliyotolewa na wahandisi wa majengo Henry Mwanaki Alinaitwe na Stephen Ekolu iliyochangia kuanguka kwa jengo moja huko Uganda mwaka 2004.
 Watu wakishuhudia jengo lililoporomoka

Haki miliki ya picha Victor Kenani, BBC
Image caption Watu wakishuhudia jengo lililoporomoka
Utafiti wao ulionesha kwamba wafanyakazi hawakuelewa kiwango sahihi cha uchanganyaji wa zege.
Utafiti huo ulisema watu walitumia matoroli bada ya vipimo stahiki kupima kiwango cha saruji.
Jengo la ghorofa tano la hoteli mpya ya BBJ iliyokuwa inajengwa ilianguka na kusababisha vifo vya watu 11.
"Utaona wajenzi na hata wafundi wanaojiita wahandisi," hayo yamesemwa na raisi wa Taasisi ya Wahandisi wa Ujenzi Nigeria, Oreoluwa Fadayomi, kwa mujibu wa gazeti la The Punch, Nigeria.
Kwa wale wanaotaka kubana hela ilihali ni wataalamu katika kazi zao: "Mtu asiwe bahili na kutumbukia kwenye upumbavu".


Aliyeshuhudia aelezea kilichotokea?

4. Jengo ni zito kuliko inavyotakikana

Bwana Ede anasema jengo huanguka wakati linakuwa zito kuliko uimara wake.
Alitoa mfano wa kumuomba mtoto ambebe kasha zito: "Bila shaka mtoto haweza kuvumilia uzito huo."
Hata kama msingi ni nyenzo zilizotumiwa ni imara, kulingana na kusudio la awali, hilo linaweza kubadilika.
Kwa hiyo, Bwana Ede anasema, ikiwa jengo lilijengwa kwa minajili ya kuwa nyumba na kisha baadaye likabadilishwa na kuwa maktaba yenye kurundikwa makasha na makasha ya vitabu, huenda uimara wa jengo hilo ukabadilika kwa sababu ya uzito ulioongezeka.
Pia aliongeza kwamba sababu nyengine inayopelekea kuwa na uzito mkubwa kuliko ilivyotarajiwa awali, ni kuongezwa kwa ghorofa nyengine tofauti na mpango wa awali.
Mnamo mwezi Machi, jengo moja lililokuwa na ghorofa nyingi kuliko lilivyopangiwa awali liliporomoka huko mjini Lagos na kusababisha vifo vya watu 34. kulingana na gazeti la the Guardian.
Hilo lilitokea miaka miwili baada ya kanisa la mhubiri mashuhuri TB Joshua kuporomoka na mamlaka ikasema sababu ni kwamba lilikuwa na ghorofa nyingi zaidi kuliko ilivyotakikana. Zaidi ya watu 100 walipoteza maisha yao.

Haki miliki ya picha Clare Spencer
Image caption Sio kawaida kuona jukwaa la mbao likijengwa nje ya jengo la kisasa kama hili lililojengwa Mwanza,Tanzania, 2016
5. Uthabiti wa jengo haufanyiwi majaribio
Kwenye kila hatua ua ujenzi wa jengo, linastahili kufanyiwa majaribio, amesema Bwana Ede.
Kuhusu sera za ujenzi wa nyumba,"Unastahili kufuata sheria,"Edo amesema.
"Sheria inasema unastahili kufanya majaribio. Utekelezaji wa sheria ndiyo tatizo," amesema.
Ameongeza kwamba kutakuwa na tatizo iwapo katika kila hatua ya ujenzi wa jengo kuna mtu anayetaka sana kubana pesa ama kuchukua kiwango fulani cha pesa.
Kuna sababu nyingi zinazochangia kuporomoka kwa jengo lakini kile kinachochochea zaidi kutokea kwa hilo ni tamaa ya pesa, amesema Bwana Ede.
Na kulingana na yeye hii ndiyo sababu kuu ya kuanguka majengo - ufisadi.
 Jukwaa la mbao katika jengo la ghorofa saba Mwanza, Tanzania, Januari 2016

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply