Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 02.05.2019: Eriksen, Felix, Fernandes, Ferdinand, Ozil, Tuanzebe
Kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27, amekubali kujiunga na Real Madrid japo hajasaini mkataba. (AS)
Menyekiti wa Spurs Daniel Levy huenda akaitisha pauni milioni £128 kumuuza kiungo huyo wa kimataifa wa Denmark. (Mirror)
- Barcelona yaicharaza Liverpool bao tatu bila huruma
- Tetesi za soka Ulaya Jumatano 01.05.2019
- Semenya ashindwa rufaa dhidi ya sheria za IAAF
Manchester United wameongeza juhudi za kuwanunua wachezaji wawili wa Urenos - mshambuliaji wa Benfica Joao Felix, 19, na kiungo wakati Bruno Fernandes, 24. (London Evening Standard)
Real nao huenda wakasubiri hadi mwaka 2020 kumsaini Eriksen kwa uhamisho wa bure. (Sun)
Mlizi wa zamani wa United Rio Ferdinand amefanya mazungumzo ya kina na klabu hi ya Old Trafford kuhusu hatua ya kufanyia marekebisho safu ya ufundi ambayo imemfurahisha naibu mwenyekiti mkuu Ed Woodward huku akipigiwa upatu kuwania wadhifa wa mkurugenzi wa kiufundia. (Manchester Evening News)
Meneja Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kumteu Mike Phelan kama mkurugenzi wa kwanza wa kiufundi. (Times - subscription required)
Kiungo wa kati wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil, 30, anasisitiza kuwa anaridhia kuwa katika klabu hiyo na kwamba anatazamia kuendelea kuwa nao msimu ujao. (Sky Sports)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino huenda akakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa vilabu vingine vya Uingereza katika soko la uhamisho wa wachezaji msimu huu wa joto. (Telegraph)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji katika kikosi cha wachezaji wa chini ya miaka 21 Charly Musonda, an matumaini ya kurejea klabu ya Vitesse msimu ujao. (Inside Futbol)
Manchester United wako tayari kumjumuisha katika kikosi cha kwanza mlinzi wa England Axel Tuanzebe, ambaye yuko Aston Villa kwa mkopo. (Mail)
Mwenyekiti wa Crystal Palace na mmiliki mwenza wa klabu hiyo Steve Parish amewahakikishia mashabiki kuwa "hatapumzika" hadi kiwango cha mchezo wao kiimarike, hali ambayo itaongeza idadi ya mashabiki katika uwanja wa Selhurst Park kutoka 26,000 hadi 34,000. (London Evening Standard)
Mlinzi wa zamani wa Arsenal abriel Paulista, 28, ambaye anajiandaa kukutana na klabu yake ya zamani katika nusu fainalii ya ligi ya Europa na anasisitiza kuwa hana chochote cha"kuthibitishia" Gunners. (Independent)
Tetesi Bora Jumatano
Real Madrid haijajiandaa kumlipa mshahara wa £290,000 kwa wiki kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba na kwamba mchezaji huyo atalazimika kuchukua kiwango cha chini iwapo anataka kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Manchester City Bernardo Silva, 24, anasema kwamba hajafikiria kuondoka katika ligi ya Premia , licha ya ripoti zinazomuhusisha na mabingwa wa Uhispania Barcelona. (Manchester Evening News)