Uchaguzi Nigeria: Kura zinahesabiwa katika uchaguzi ulioahirishwa
Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Nigeria kufuatia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo,Hata hivyo upigaji kura ulisogezwa kufikia siku ya pili katika maeneo machache
Kutokana na hitilafu ya mambo,kutokukamilika kwa mipango na vurugu katika baadhi ya maeneo uchaguzi umesogezwa mpaka hapo baadae.
Raisi Muhamadu Buhari mwenye miaka 76 anatetea kiti chake kwa awamu ya pili .Mpinzani wake mkuu ni Makamu wa Rais wa zamani Atiku Abubakar, 72.
- Upinzani washinikiza kuachiliwa kwa Halima Mdee Tanzania
- Raia wa Senegal wapiga kura
- Saudia yamchagua bintimfalme kuwa balozi wake Marekani
Uchaguzi ulitakiwa kufanyika juma moja lililopita na baadae kuahirishwa katika dakika za lala salama
Kwa yeyote atakeshinda na kukikalia kiti hicho katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi Barani Afrika na uchumi mkubwa atakabiliwa na suala la ukosefu nishati ya uhakika,Rushwa ,tishio la kiusalama na kuporomoka kwa uchumi.
Rais Buhari alipiga kura yake katika mji wa Daura kaskazini mwa mkoa wa Katsina.Alipoulizwa kama atampongeza mpinzani wake pale atakapoangushwa kwenye uchaguzi huo alisema. ''Nitajipongeza Mwenyewe''
Bwana Abubakar,Mfanyabiashara Mkubwa ,Amesema ana Imani ya kushinda uchaguzi.
Huenda matokeo yakatangwazwa siku ya Jumatatu
Uchaguzi ulikua wa Amani?
Sehemu kubwa ya nchi hiyo ilionekana kua katika utulivu lakini kumekua na taarifa za uwepo wa Kundi la wapiganaji la Boko Haram eneo la kaskazini,Wapiga kura walitishwa huku wakijaribu kutaka kuiba masanduku ya kura katika sehemu ya vituo Hasa katika mikoa ya Kaskazini , Lagos na Anambra.
Muungano wa makundi ya asasi za kiraia umeripoti kua jumla ya watu 16 waliuawa -Idadi mbayo ni ndogo ikilinganiswa na uchaguzi Uliopita
Watu wawili walitiwa kizuizini katika mkoa wa Surulere eneo la mji mkubwa wa kibiashara Lagos , baada ya wapiga kura kuvamiwa na kundi la vijana wadogo Wakiwa na silaha kama jambia,shoka na Vitu vyenye ncha kali , Shuhuda mmoja aliiambia BBC.
Tume ya Uchaguzi yenyewe inasema kua uchaguzi haukuwezekana katika vituo 8,500 kati ya vile 120,000 katika eneo lote la nchi ,Shirika la Habari la AFP Limeripoti.
Mgombea atakayepata kura nyingi atatangazwa kua mshindi katika duru ya kwanza ya uchaguzi ,Hii ikiwa atapata asilimia 25% ya kura katika mbili ya tatu ya majimbo 36
Wagombea wa nafasi ya uraisi walikua 73 ,lakini ushindani mzito Zaidi ulishuhudiwa kati ya raisi wa sasa Muhamadu Buhari na mfanyabiashara mkubwa Nchini Humo Atiku Aboubakar