Lawrence Okettayot yuko njiani kuizunguka nchi yote ya Uganda.
Anaeneza habari kuhusu kifaa alichovumbua kinachoweza kutatua tatizo la kuharibika chakula Afrika.
Chakula kinachoharibiwa kila mwaka kinaweza kuwalisha watu milioni 300 kulingana na umoja wa mataifa. Katika taifa la Uganda pekee, hadi asilimia 40 ya matunda na mboga uharibika.
Lakini Lawrence, 23, ana matumaini kwamba uvumbuzi wake wa Sparky Dryer utabadilisha kila kitu.
The device is a dehydrator running on garden waste that dries fruits and vegetables quickly, making them last for months instead of days, generating zero carbon emissions.
Kifaa hicho kinakausha matunda na mboga kwa haraka, ili vyakula hivyo vipate kukaa kwa muda mrefu bila kutoa gesi yoyote ya kaboni.
Kinafanana na jokovu dogo na kinatumia taka za shambani badala ya umeme, ambapo ni wakulima wachache nchini Uganda wanaomiliki kifaa hicho.
Chakula kinachooza
Chakula kingi kinachouzwa masokoni uharibika kwa sababu wakulima hawawezi kukihifadhi. Hivyo basi wanalazimika kurudisha nyumbani ili kuvuna matunda mapya na mbogo kuuza siku inayofuata.
Wakati wa msimu wa kiangazi ni chakula kichache hukua hapa hivyo basi watu wengi hukumbwa na njaa, anasema Lawrence wakati alipokuwa akitembelea katika soko hilo lenye biashara nyingi katika jimbo la kaskazini la Kitgum, akipita vibanda vidogo na mirundiko ya chakula kilichoharibika
Bei ya chini ya Sparky Dryer moja ni $80. Na kila kifaa kinaweza kukausha kilo 10 za maembe kwa saa mbili.
Ina eneo dogo ambapo moto wa gesi huwekwa ili kutoa joto katika eneo linalotumiwa kukausha ambapo chakula hicho hupangwa. Pia kuna inayotumika kuzuia gesi hatari kutotoka wakati wa ukaushaji.,
Mbali na Sparky Drier kuna vifaa vya kukausha vinavyotumia umeme ambavyo ni ghali , huku mbinu za kukausha za kitamaduni kama vile kutumia jua haziwezi kutumika vyema wakati wa msimu mvua na huchukua muda mrefu
Lakini licha ya uwezo wake , Lawrence amefanikiwa kuuza vifaa vichache- 7 pekee. Je uvumbuzi wake unafanya kazi?
Umbali wa safari ya saa tatu barabarani kutoka Kitgum, anaishi Joe Okettayot, mjombake Lawrence ambaye ni mmoja wa wakulima ambaye ameleta kifaa hicho cha kukausha
Lawrence alipata msukumo wa kuwa na wazo hilo baada ya mjombake kumwambia alikuwa na mpango wa kuwacha kilimo
''Tulikuwa tukitupa chakula kingi tulichokuwa tukipanda…''
Sasa tunaweza kukausha maembe na matunda mengine hata wakati kuna mvua ,hivyobasi hatutupi chochote tena.
Tunauza bidhaa zilizokaushwa wakati wa msimu wa joto mara nne Zaidi ya kiwango cha mazao mapya''. Joe anaongezea huku akiotesha nyumba ya matofali aliyojenga katikati ya shamba lake kwa kutumia mapato yake ya ziada.
Mamlaka imekiri kwamba wana tatizo kubwa la uharibifu wa chakula lakini imeshindawa kupata suluhu
''Tuna viwanda viwili pekee vya kusindika chakula'', alisema james Tumwine kutoka wizara ya Kilimo
Serikali haifanyi biashara na wawekezaji wa kibinafsi hawana habari kuhusu fursa iliopo .wanapanga kuanzisha maeneo ya kusindika chakula kwa bidhaa maalum katika maeneo tofauti, lakini wanasindika polepole.
Ukirudi Kitgum , Lwarence , Lawrence ana matumaini kuhusu hatma ya siku zijazo na anataka kuimarisha uvumbuzi wake kufikia maeneo mengine ya dunia.
This BBC series was produced with funding from Bill & Melinda Gates Foundation